Posts

Showing posts from December, 2015

MKUNGA care: UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA SIKU ZA HATARI KUPA...

MKUNGA care: UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA SIKU ZA HATARI KUPA... : Utoaji mimba usiosalama umekuwa ukiongezeka hapa nchini kutokana na kupata mimba zisizitarajiwa hasa katika umri mdogo.Tatizo kubwa ni ukose...

UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA SIKU ZA HATARI KUPATA MIMBA

Image
Utoaji mimba usiosalama umekuwa ukiongezeka hapa nchini kutokana na kupata mimba zisizitarajiwa hasa katika umri mdogo.Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu sahihi juu ya siku za hatari kushika  mimba katika mzunguko wa siku za hedhi. Makundi matatu ya mzunguko wa hedhi :  mzunguko mfupi ambao uchukua siku 25 na pungufu. mzunguko wa kawaida,siku 28 mzunguko mrefu, ambao ni mpaka siku 35 Tambua mzunguko wako: Ili uweze kutambua mzunguko wako unachukua siku ngapi yakupasa kuanza kuhesabu tangu siku ya kwanza umeanza kuona damu mpaka tarehe utakapoona damu tena katika mwezi unaofuata.Fanya hivyo kwa miezi 3 mpaka 6 ili uweze kuona kama mzunguko wako haubadiliki.   Siku za hatari: Kwa mwenye mzunguko wa kawaida(siku 28) siku ya kumi na nne(14) ndio siku ya utoaji wa yai la kike(ovulation),hivyo ukifanya ngono siku ya 14 kuna uwezekano mkubwa wa kupata mimba,pia kuanzia siku ya 11 , 12 na 13 upo uwezekano wa kupata mimba,pamoja na siku ya 15 , 16 na 17 .Hivyo ...