UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA SIKU ZA HATARI KUPATA MIMBA

Utoaji mimba usiosalama umekuwa ukiongezeka hapa nchini kutokana na kupata mimba zisizitarajiwa hasa katika umri mdogo.Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu sahihi juu ya siku za hatari kushika  mimba katika mzunguko wa siku za hedhi.

Makundi matatu ya mzunguko wa hedhi:

  1.  mzunguko mfupi ambao uchukua siku 25 na pungufu.
  2. mzunguko wa kawaida,siku 28
  3. mzunguko mrefu, ambao ni mpaka siku 35
Tambua mzunguko wako:
Ili uweze kutambua mzunguko wako unachukua siku ngapi yakupasa kuanza kuhesabu tangu siku ya kwanza umeanza kuona damu mpaka tarehe utakapoona damu tena katika mwezi unaofuata.Fanya hivyo kwa miezi 3 mpaka 6 ili uweze kuona kama mzunguko wako haubadiliki.  

Siku za hatari:
Kwa mwenye mzunguko wa kawaida(siku 28) siku ya kumi na nne(14) ndio siku ya utoaji wa yai la kike(ovulation),hivyo ukifanya ngono siku ya 14 kuna uwezekano mkubwa wa kupata mimba,pia kuanzia siku ya 11,12 na 13 upo uwezekano wa kupata mimba,pamoja na siku ya 15,16 na 17.Hivyo siku hizo zote ni siku za Hatari.


Lakini ikumbukwe hii ni kwa mwenye mzunguko wa siku 28.

Kwa mzunguko mfupi,mfano mzunguko wa siku 21, ili kujua siku za Hatari chukua 21 toa 14, utapata saba (7),hivyo siku ya 4,5,6,na 7 ni siku za hatari pamoja na siku ya 8,9 10.

Pia kwa mzunguko mrefu mfano siku 35utatoa kumi na nne (14), utapata 21 maana yake siku ya 21,ni hatari pamja 17,18,19,20 ,22,23 na 24.

Comments

Popular posts from this blog